Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA-, Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kupitia ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa kijamii wa X, amekanusha taarifa za kufutwa kwa mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani.
Araqchi: Mazungumzo na Marekani yatafanyika Ijumaa mjini Muscat
Katika ujumbe wake aliandika:
“Inatarajiwa kuwa mazungumzo ya nyuklia na Marekani yatafanyika siku ya Ijumaa takribani saa 4:00 asubuhi (saa za Muscat). Nawashukuru ndugu zetu wa Oman kwa kufanya maandalizi na uratibu wote unaohitajika.”
Vyombo vya habari vya kimataifa vilikuwa vimeripoti mapema kuwa mazungumzo yajayo kati ya Iran na Marekani yamefutwa, wakidai kuwa sababu ni upinzani wa Iran kujadili masuala yasiyo ya nyuklia.
Hata hivyo, vyanzo vya Iran viliviambia leo gazeti la Al-Araby Al-Jadeed kuwa misimamo ya Marekani katika siku za hivi karibuni imekuwa ikibadilika-badilika. Ripoti hiyo ilieleza kuwa Marekani, chini ya shinikizo la Israel na makundi yenye mwelekeo wa vita, inajaribu kubadili mfumo wa mazungumzo na kuingiza masuala yasiyo ya nyuklia katika ajenda ya mazungumzo.
Your Comment